Mafunzo kwa makarani waongozaji katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mfaranyaki yanaendelea kutolewa leo tarehe 15 Septemba 2023 kwa washiriki, yanayofanyika katika ukumbi wa SACCOS ya Watumishi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kutoa elimu ya uelewa juu ya majukumu yao wakati wa zoezi lka uchaguzi.
Mafunzo hayo yatafanyika katika makundi mawili ikiwemo kundi la Mkarani waongozaji pamoja kundi la pili ni la wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ambao mafunzo yao yatafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 17 Septemba 2023.
Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Mfaranyaki utafanyika tarehe 19 Septemba 2023 siku ya jumanne.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa