• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAJALIWA azindua X RAY ya kidigitali Hospitali ya Rufaa Songea

Tarehe ya kuwekwa: January 6th, 2019

Waziri Mkuu amezindua mpango wa usambazaji wa x-ray za kidigitali ambazo zitazambazwa kwenye hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa ili kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa kwa njia ya mionzi.Waziri Mkuu amesema kwa kuanzia x-ray hizo zitasambazwa kwenye hospitali za rufani katika mikoa 11 na kisha baadae zitasambazwa kwenye hospitali zingine 20, lengo ni kuhakikisha hospitali zote za rufaa za mikoa zinakuwa na x-ray hizo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ndungulile amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za nchini.Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote karibu na maeneo yao ya makazi tena kwa gharama nafuu. ”Katika kufikia azma hii moja wapo ya kipaumbele ni kununua vifaa vya kisasa vinavyoendana na teknolojia iliyopo.”

Amesema kwa sasa wizara hiyo imenunua mashine 11 za x-ray za kidigitali zenye thamani ya zaidi ya shilingi 2,027,029,794.60 ambazo zimekusudiwa kupelekwa kwenye hospitali 11 zenye x-ray za zamani. Hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Singida na zingine tatu zitafungwa katika hospitali za wilaya za Chato, Magu na Nzega. 

Wakati huo huo  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto  katika Hospitali ya Rufaa  ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.Waziri Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019) wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni 129.“Sijaridhishwa na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara, jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi inalingana na thamani ya fedha.Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati wanatakiwa watibiwe bure.Waziri Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.Pia baada ya Dkt. Ndungulile kuangalia cheti cha mtoto huyo alisema dawa aliyoandikiwa ipo hospitalini hapo jambo ambalo lilithibitishwa na Mganga Mfawidhi wa hopitali hiyo Dkt. Majura Magafu, hivyo Waziri Mkuu amemuagiza mganga huyo amtafute mtendaji.

TAARIFA imetolewa na Blogu ya Waziri Mkuu

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa