Makamu Mwenyekiti TALGWU Taifa Romward Mwashiuya amewataka watumishi Mkoani Ruvuma kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yote ya kiutumishi wa umma.
Chama cha TALGWU hakitafurahishwa na hakitapendezwa kusikia uwepo wa watumishi ambao hawatekelezi majukumu yao vizuri kwa kutegemea kuwa watasimamiwa na chama kitendo ambacho kinaashiria kwamba mahala penye kesi nyingi watumishi wake wanamatatizo ambapo Chama hicho hakitatetea mtumishi mzembe.
Hayo yamejili katika kikao cha wanachama wa TALGWU Wilaya ya Namtumbo akiwa kwenye ziara ya kutembelea wanachama kwa lengo la kusikiliza kero za wanachama iliyofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 25 Novemba 2022 ambapo alitembelea Wilaya ya Namtumbo na Nyasa Mkoani Ruvuma.
Mwashiuya alisema “ Serikali ni sikivu sana imeweza kupokea hoja kutoka kwa vyama vya wafanyakazi na kuzitatua ikiwemo na kupandisha madaraja kwa watumishi, nyongeza ya mshahara, na kuwalipa watumishi waliondolewa kazini kwa kughushi vyeti . “ alipongeza”
Amewataka watumishi Mkoani Ruvuma kukusanya mapato ya Serikali pamoja na kusimamia kutekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kufuata taratibu za manunuzi ya vifaa vya Serikali na kuachana na tabia ya ukiukwaji wa maadili.’ Mwashiuya alisisitiza”
Akieleza bayana juu ya T-shirt za Mei Mosi 2022 alisema Chama cha TALGWU kilitenga fedha Bil. 1.2 kwa ajili ya kutengeneza T-shirt ambapo Shilingi Mil 700 alikabidhiwa Mzabuni na baada ya kubaini mapungufu ya T-shirt zilizoletwa sio sahihi kama makubaliano yaliyopangwa, Chama kiliamua kusitisha mkataba huo na kuandaa T-shirt kwa Mzabuni mwingine ambapo alikabidhiwa kiasi cha shilingi Mil. 300 ambazo zilivaliwa siku ya sherehe za Mei Mosi na kuwa na bakaa ya shilingi Mil.200.
Aliongeza kuwa kutokana na chanagamoto iliyojitokeza kwa mwaka huu chama hakitagawa T-shirt bali TALGWU imejipanga kuandaa T-shirt nyingine ambazo zitagawiwa ifikapo Mei Mosi 2023 pamoja na zawadi nyingine mmbadala ya T-shirt ya mwaka 2022. “Mwashiuya alibainisha.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa RUVUMA Willey Luambano alisema jukumu la viongozi Mkoa wa Ruvuma ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa wanachama ili kuilinda ajira na utumishi kwa lengo la kuondoa migogoro mahala pa kazi.
Willey alisema Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wananchama hai 2900 ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nammtumbo imefanikiwa kusimamia na kushinda mashauri ya kinidhamu kwa watumishi 12 ambapo aliwarai wanachama hao kufanya kazi kwa kufuata misingi ya Serikali.
Naye Mwenyekiti wa Uratibu TALGWU Wilaya ya Namtumbo Maximilian Komba alisema Wilaya ya Namtumbo ina zaidi ya matawi 17 ambapo amewataka wenyeviti wa matawi Wilayani humo kufanya vikao vya kikatiba kwenye matawi husika ili kusikiliza kero za wanachama ikiwemo na kutatua migogoro ya wanachama.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka PSSSF Daniel Herman alisema PSSSF imeundwa kwa sheria namba 2 ya mwaka 2018 yenye lengo kuunda mfuko ni kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma.
Herman aliongeza kuwa kuna mafao ya aina saba 7 ambayo ni mafao ya uzeeni, mafao ya kifo, mafao ya warithi, mafao ya ulemavu, mafao ya ugonjwa, mafao ya kukosa ajira pamoja na mafao ya uzazi ambapo alisema pesheni hiyo hulipwa kwa mwanachama aliyechangia miezi 180 na ameondoka na ajira kwenye akiwa na umri chini ya miaka 55 kwa sababu ya kuchaguliwa/kuteuliwa katika nafasi za kisiasa, kustaafishwa kwa manufaa ya umma, kupunguzwa kazi, mabadiliko yay a kimuundo wa taasis, na kufutwa kwa taasis.
Akifafanua kuhusu kikokotoo ambapo alibainisha kuwa mafao yatakuwa 1/580*idadi ya miezi aliyotumikia* wastani wa mshahara wa mwaka pia alisema mafao ya mkupuo yatakuwa 1/580*idadi ya miezi aliyotumikia*wastani wa mshahara wa mwaka *12.5*0.33 pamoja na mafao ya pesheni ya kila mwezi 1/580*idadi ya miezi aliyotumikia * wastani wa mshahara wa mwaka*0.67*1/12.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa