HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea kupitia program ya maji na usafi wa mazingira inaendelea kukarabati visima vya maji 89 lengo ni kuongeza utoaji huduma ya maji kwa wananchi.Mradi huo unaotekelezwa katika kata 10 unagharimu zaidi ya shilingi milioni 294.Hadi sasa visima 61 vimekarabatiwa bado visima 28.
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekagua visima vilivyokarabatiwa na kubaini visima vyote vinatoa maji na wananchi wanafurahia huduma ya maji jirani na maeneo ambayo wanaishi.Hata Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ameagiza Idara ya Maji katika Manispaa hiyo kukamilisha haraka ukarabati wa visima 28 vilivyobakia ili kumaliza kero kwa wananchi wa maeneo husika ikiwemo kata ya Subira ambayo haijakarabatiwa hata kisima kimoja.
Visima vilivyokarabatiwa ni vya muda mrefu tangu kujengwa kwake miaka ya 1985 na 1992 ambavyo miundombinu yake ya ndani ya visima imechakaa hivyo kushindwa kutoa maji kwa wananchi.Ukarabati wa visima hivyo umeanza tangu Februari 2018 ambapo hadi sasa visima 61 vilivyokarabatiwa vinatoa maji na kwamba Idara ya Maji kupitia watalaam wake wanaendelea kukarabati visima 28 vilivyobakia lengo ni kukamilisha visima vyote 89 ili huduma ya maji kwa wananchi ipatikane kwa wakati.
Mchanganuo wa visima vilivyokarabatiwa unaonesha kuwa katika kata ya Lilambo visima vinavyokarabatiwa ni 16,Tanga visima 20,Metele visima vitatu ,Seedfarm visima viwili,Ruhuwiko visima 14,Mshangano visima viwili na Kata ya Ruvuma visima vinne.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 27,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa