HALMAHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ilipokea fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Tshs. 400,000,000.00 Kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Ruvuma mnamo tarehe 24.06.2018. Taratibu za Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Ruvuma ulianza tarehe 24/07/2018 baada ya kupata michoro kutoka OR-TAMISEMI. Mradi unatarajiwa kukamilika wakati wowote. Mpaka sasa mradi huu umegharimu jumla ya Tshs. 217,810,141.63. Utekelezaji wa mradi huu ni zaidi ya asilimia 90.
UJENZI UNAOTAKIWA KUFANYIKA:
1. Jengo la Upasuaji (Theatre)
2. Wodi ya Kina mama (Maternity block)
3. Maabara (Laboratory)
4. Jengo la mapokezi (Out Patient Department)
5. Kichomea taka (Incinerator)
6. Shimo la kutupia kondo la nyuma (Placenta pit)
7. Shimo la kuhifadhia maji taka (Soak away pit)
KAZI ZILIZOFANYIKA MPAKA SASA:
1. Jengo la OPD limekwisha ezekwa, kuwekwa mfumo wa awali wa umeme, Maji, kupiga brandering, kupigwa plasta, kupachika frame za milango na kufanya curing
2. Jengo la Maternity limeezwa, limepigwa brandering, kuwekwa mfumo wa awali wa umeme kazi ya kupigwa Lipu imekamilika kwa sasa kazi ya kupachika frem za milango inaendelea pamoja na kupiga koplo.
3. Jengo la Theatre limeezekwa, limewekwa mfumo wa awali wa umeme, kazi zinazoendelea kwa sasa ni kupiga Lipu, brandering na kupachika magrill
4. Jengo la Maabara limeezekwa,limepigwa brandering,mfumo wa awali wa umeme na maji,limepachikwa magrill,limepigwa Lipu,kazi inayoendelea kwa sasa ni kupachika frem za milango na koplo.
5. Kazi ujenzi wa shimo la choo na shimo la kondo la nyuma zimekamilika
6. Kazi za ujenzi wa kichomeataka ipo kwenye hatua ya ukamilishaji.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa