HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefaulisha kwa asilimia 79 katika mtihani wa Taifa wa shule za msingi uliofanyika mwaka 2018.
Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Songea Gerald Chavallah akizungumza ofisini kwake mjini Songea katika mahojiano maalum amesema mwaka 2019,Halmashauri hiyo inatarajia kufanya vizuri zaidi ambapo katika matokeo ya MOCK imefaulisha kwa asilimia 83.
“Matokeo ya mwaka 2018 tumefaulisha kwa asilimia 79 katika Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekuwa ya tatu na mtihani wa moko kwa mwaka 2019 tumefaulisha kwa asilimia 83”.amesema Chavallah
Kaimu Afisa Elimu hiyo ameitaja mbinu zitakazosaidia kuongeza ufaulu wa darasa la saba, mwaka 2019,kuwa ni walimu kufundisha katika muda wa ziada, kutoa mazoezi mengi na wazazi kuhamasika kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi wapate muda wa kutosha wa kukaa shuleni kuendelea kujifunza.
Kila mwaka Halmashauri ya Manispaa ya Songea yenye shule za msingi 99, imekuwa inaongoza katika mtihani wa Taifa katika shule za msingi mkoani Ruvuma kati ya Halmashauri nane zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma.
Imeandaliwa na
Jamila Ismail
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 2, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa