MATUMIZI ya dawa za kulevya hasa kwa vijana bado ni tatizo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kama ilivyo kwa nchi nzima. Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2017 Manispaa ilikuwa na Waathirika wa dawa za kulevya waliojitokeza kupata huduma 106 kati ya hao Wanaume ni 105 na Mwanamke ni mmoja.
Katika kipindi cha Januari hadi Mei, 2018 Manispaa ya Songea ina jumla ya waathirika wa dawa za kulevya waliojitokeza kupata huduma wapatao 108 wote wakiwa ni Wanaume wenye umri kati ya miaka 15 – 62. Manispaa ya Songea inatoa Wito kwa Wananchi wote kutojihusisha kwa namna yeyote kutumia dawa haramu za kulevya.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike anawashauriwa wale walioathirika na dawa za kulevya kwenda kwenye vituo vya Afya kupata tiba na ushauri nasaha.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 18,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa