MPAKA kufikia Juni, 2018, upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 50.1 sawa na idadi ya watu 45,929 kwa wakazi waishio pembezoni mwa Mji wa Manispaa ya Songea yaani sehemu ambazo Mamlaka ya Maji safi na Taka (SOUWASA) hawajaweza kutoa huduma ya Maji safi na Salama.
Mkuu wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya anasema Halmashauri mwaka 2007 wakati inaanza kutekeleza programu ya maji ilikuwa na asilimia 17 tu na kwamba tangu mwaka 2007 inaendelea Kutekeleza Programu ya maji na Usafi wa Mazingira katika Mitaa 10 ,awamu ya kwanza ambayo ni Mahilo, Chandarua, Muhombezi, Muungano, Mahinya, Ngandula, Ruhuwiko Kanisani, Mitendewawa, Ruhila kati na Liwumbu.
Hata hivyo anasema Mpaka kufikia mwaka 2018, Utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya maji,awamu ya kwanza umekamilika kwa asilimia 95. Mitaa ya Mitendewawa na Ruhila Kati ujenzi wa miundombinu ya maji upo hatua za mwisho za ukamilishaji. Mtaa wa Liwumbu ulikosa chanzo cha maji kabisa kutoka ardhini (ground water).
Kulingana na Mhandisi Sanya, Halmashauri imeendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya maji kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira (phase II) katika Mitaa ya Mwengemshindo, Pambazuko, Mletele, Mjimwema, Makemba, Mdundiko, nonganonga, Liwumbu, Nangwahi,Subira Kati,Kisiwani C, Lami na Kihekwa.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 22,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa