HALMASHAURI ya Manispaa Songea mkoani Ruvuma ina jumla ya viwanda 512 vilivyopo katika baadhi ya kata zilizopo katika Halmashauri ya manispaa hiyo.
Kati ya viwanda hivyo kiwanda kikubwa ni kimoja ambacho ni cha kusindika tumbaku kinachomilikiwa na Chama cha Ushirika cha SONAMCU ambacho kwa sasa hakifanyi kazi na mchakato wa kukifufua unaendelea.
Viwanda vingine ni viwanda vya kati ambavyo vipo tisa, viwanda vidogo vipo 132 na viwanda vidogo sana ni 371.
Hata hivyo viwanda hivyo vya kati,vidogo na vidogo sana ni vya kukamua mafuta ya alizeti, usindikaji wa Mihogo, usindikaji wa mboga mboga na Matunda, kukoboa Mpunga na viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka.
Katika hatua nyingine ya maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepima viwanja 150 katika eneo la kata ya Lilambo kwa ajili ya uwekezaji hususani kwenye sekta ya viwanda.
Hivi sasa Halmashauri ya Manispaa ya Songea inaandaa mradi wa kimkakati ili kujenga soko la kisasa la Manzese ambalo litaboresha huduma kwa wananchi pamoja na kuiletea mapato Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Septemba 14,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa