HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, imeendelea kuwakumbusha wadau wote wa mapambano dhidi ya rushwa, kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais wetu Mh. Dkt John Pombe Magufuli za kuchukua hatua dhidi ya Rushwa.
Katika kipindi cha Januari hadi Mei 2018 jumla ya taarifa 12 za matukio ya rushwa zimeripotiwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kufanyiwa kazi na kusababisha kufunguliwa kesi tatu Mahakamani.
TAKUKURU katika Manispaa ya Songea imefanya tafiti sita kuhusu rushwa ili kubaini mianya ya Rushwa kwenye Idara mbalimbali za serikali. Aidha Manispaa ya Songea kwa kushirikiana na TAKUKURU imeelimisha jumla ya Wananchi 1,300 na kutoa machapisho zaidi ya 920 Kuhusu Rushwa.
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Pia zimefunguliwa klabu 17 za kuelimisha na kupambana na rushwa Mashuleni.
MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA: “Kataa Rushwa Jenga Tanzania ”
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa