Katika kupambana na udumavu pamoja na utapiamlo, kitengo kimefanya uchunguzi wa hali ya lishe kutumia mzingo wa mkono kwa watoto chini ya miaka mitano na kubaini hali ya utapiamlo kufikia asilimia 0.08 hadi septemba 2020.
Hayo yamebainishwa na kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Beno Philipo katika kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 09 novemba 2020.
Beno alisema ili kuondoa au kupunguza idadi ya utapiamlo ndani ya Manispaa ya Songea tunapaswa kutoa elimu kwa jamii namna ya uandaaji wa chakula lishe kwa mtoto chini ya miaka mitano, mpangilio wa ulaji wa chakula, na aina ya chakula kinachofaa kuliwa.
Naye kaimu mganga Mkuu Manispaa ya Songea Dr. Beda Mgegedu alibainisha kuwa katika kipindi cha julai hadi Septemba kitengo cha uchunguzi wa hali ya lishe kutumia mzingo wa mkono chini ya miaka mitano ni jumla ya watoto 27,640 walichunguzwa, na kati ya hao waliogundulika kuwa na utapiamlo mkali ni 23 sawa na asilimia 0.08, na waliogundulika kuwa na utapiamlo wa kadiri ni 116 sawa na asilimia 0.4, na watoto waliogundulika kuwa hawana utapiamlo 27, 501 sawa na asilimia 99.4.
Miongoni mwa mikakati waliyojiwekea ili kupambana na hali ya utapiamlo ni kutoa elimu kwa jamii kwa kuitisha mikutano ya hadhara mashuleni/ mitaa pia kupitia vyombo vya habari, kuzitembelea shule pamoja na kamati za shule ili kuongeza ushirikishwaji na kukabiliana na utapimlo Wilayani humo ” Dr. Mgegedu alisema.
Aidha, Utaoji wa fedha za mikopo kwa jamii ya Wanawake, Vijana, na Watu wenye ulemavu unaendelea kutolewa kwa nia ya kuongeza nguvu ya kiuchumi katika miradi yao na kuwezesha upatikanaji wa fedha ya lishe, ambapo jumla ya vikundi 48 walipatiwa mikopo ikiwa vikundi vya wanawake 25 walipata mikopo 43,476,777.9099, vikundi vya vijana 27 walipata mkopo wa tsh 43,467,777.9099 na vikundi vya walemavu 6 walipata mkopo milioni 15,733,886.00 ili kutatua masuala ya lishe kwa kuhamasisha wanawake kuhusiana na shughuli za kiuchumi na kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora.” Alisema afisa maendeleo ya jamii Judith Ngowi”
Naye Afisa Mifugo Manispaa ya Songea Rozina Chuwa alisema Idara ya mifugo inaendelea kutoa Elimu juu uzalishaji wa malisho, na uandaaji pamoja uhifadhi wa malisho kwa vikundi 13 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa uandaaji na uhifadhi wa malisho ili kuisaidia jamii katika kujiongezea kipato na kuwa najamii yenye lishe bora.
Mwisho, waliipoingeza Serikali kwa zoezi la unyweshaji wa dawa za kinga tiba kwa magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo pamoja na usambazaji wa vyandarua kwa shule za Msingi kwa madarasa ya V, VI na VII.” Alibainisha Afisa elimu Fideilis Kidungu”
MTAYARISHAJI;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
10 Novemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa