• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Manispaa ya Songea Kupambana na Utapiamlo.

Tarehe ya kuwekwa: May 3rd, 2021

Lishe bora ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kiweze kusaidia mwili kukua vyema kwa afya njema na kuweza kupigana na magonjwa mwilini pia  Utapiamlo ni lishe mbaya na hutokea ikiwa unakula chakula kidogo sana au kingi sana au kula chakula kisichokuwa na lishe ya kutosha.

Miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula Tanzania ni pamoja na Mkoa wa Ruvuma, licha ya ongezeko hilo la chakula bado kumekuwepo na tatizo la utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano.

Tathimini ya utekelezaji wa kamati ya lishe Manispaa ya Songea kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021 kiwango cha watoto wenye utapiamlo kimepanda kutoka asilimia 0.1% Oktoba hadi Disemba 2020 na kufikia asilimia 0.2% Januari hadi Machi 2021 ambapo jumla ya watoto 24 kati ya watoto 37,502 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali ukilinganisha na kipindi cha Robo mwaka iliyopita Oktoba hadi Disemba 2020 ambapo watoto 21 kati ya watoto 36,748 wenye umri chini ya miaka mitano waliogundulika kuwa na utapiamlo.

Ongezeko hilo la watoto wenye utapiamlo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021, ni kutokana na baadhi ya wazazi kujishughulisha na shughuli za kilimo kwa kipindi cha masika ya mvua na kuacha watoto bila chakula cha kutosha kwenye  kaya zao.

Hayo yameelezwa na kamati ya lishe Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa zoezi la lishe katika kipindi cha Robo mwaka Januari hadi Machi 2021 iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo tarehe 3 Mei 2021.

Wakibainisha baadhi ya changamoto zinazopelekea ongezeko la watoto wenye utapiamlo wenye umri chini ya miaka mitano ni pamoja na uhaba wa chakula dawa (RUTF) katika vituo vya Afya na baadhi ya watoa huduma katika vituo vya Afya kutokuwa na uelewa juu ya elimu ya lishe.

Ili kukabiliana na changamoto hizo Manispaa ya Songea imejipanga kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, kuundwa kwa kamati za lishe mashuleni, Wataalamu wa Afya kuelimisha namna ya uandaaji wa lishe bora kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kuhakikisha akina mama wajawazito wanahudhuria kliniki mara anapohisi ana ujauzito,  Kutumia sheria ndogo za lishe, watendaji wa kata/ mtaa kufuatilia kaya zenye watoto wenye utapiamlo, kuhakikisha kila shule inatengeneza bustani za mboga mboga na kupanda miti ya matunda, pamoja na kutolewa kwa mafunzo maalumu ya uandaaji wa chakula cha lishe kwa wanafunzi mashuleni.

IMEANDALIWA NA,

AMINA PILLY,

AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA,

3/05/2020.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa