Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano amewataka wananchi kuwa na uzalendo wa kuwatembelea watu wenye mahitaji maalumu na kuwafariji ili kujenga uzalendo.
Amesema hayo wakati tarehe 24 desemba 2024 alipowatembelea mahabusu na wafungwa pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu kwa lengo la kuwafariji na kuwapa zawadi katika kipindi cha Krismas na mwaka mpya.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa wahitaji hao ni Ng’ombe mmoja, mbuzi mmoja, Mchele kg 200, Maharage 70, Magodoro 20, pamoja na Mafuta ya kula.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa