NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
29.10.2021
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeweka mkakati wa kutenga bajeti kwa kutoa shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 kwa lengo la kutekeleza afua ya mkataba wa lishe ndani ya Manispaa ya Songea.
Hayo yamebainishwa na Andambike Kyomo - Mchumi Manispaa ya Songea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kamati hiyo kilichofanyika leo tarehe 29 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za lishe robo ya kwanza kwa kipindi cha Julai hadi Septemba kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Akizungumza katika kikao hicho Kyomo ametoa wito kwa kamati ya lishe Manispaa ya Songea kusimamia shughuli za lishe kwa ukamilifu hasa kwa watoto wenye umri wa miaka 5 pamoja na watoto waliopo mashuleni wenye umri chini ya miaka 18 .
Amewataka wanakamati hao kufuatilia takwimu zinazotolewa kwenye taarifa na kuzilinganisha na uhalisia wa hali ya lishe ulivyo hasa kwenye maeneo ya shule za Msingi ndani ya Manispaa ya Songea ikiwemo na hali ya utoaji chakula kwa wanafunzi kwa muda wanapokuwa shuleni.
Kwa upande wake Afisa lishe Manispaa ya Songea Florentine Kissaka alisema kuwa jumla ya watoto 32234 wenye umri wa chini ya miaka mitano walichunguzwa hali ya lishe kati ya watoto 31512 ambayo ni sawa na asilimia 102.3% ambapo kati ya watoto hao 29 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali ambao ni sawa na asilimia 0.1%.
Aliongeza kuwa watoto 31450 wenye umri chini ya miaka mitano ambao ni sawa na asilimia 97.6% waliochunguzwa hawakuwa na utapiamlo ambapo watoto waliogundulika kuwa na utapiamlo walipewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa kwenda hospitali ya rufaa Songea kwa ajili ya kupatiwa matibabu.”Kissaka alibainisha “
Alisema kuwa kamati imejipanga kutembelea kata 21 za Manispaa ya Songea kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuandaa lishe bora pamoja na kuwahamasisha wazazi wenye watoto mashuleni umuhimu wa kuchangia chakula kwa watoto wanapokuwa shuleni ambapo hadi sasa shule za msingi 30 kati ya shule 50 zilizotembelewa zinatoa chakula shuleni (Idadi ya shule za msingi Manispaa ya Songea ni 92) ambapo hadi kufikia Januari 2022 shule zote zinatakiwa kutoa chakula kwa wanafunzi muda wote wa masomo.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa