• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA YA SONGEA YAFANIKIWA KUCHANJA CHANJO YA POLIO ZAIDI YA 100%

Tarehe ya kuwekwa: September 9th, 2022

Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanikiwa kutekeleza zoezi la utoaji wa Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka mitano 5 kwa  zaidi ya asilimia 100%   kwa awamu zote tatu za utekelezaji wa zoezi hilo.

Kauli hiyo imetamkwa leo tarehe 09 Septemba 2022 katika kikao cha PHC ambacho hufanyika pale ambapo kuna utekelezaji wa jambo linalohusu afya ambacho kilihudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Kamati za Elimu, Afya na Uchumi, wataalamu wa Afya na wakuu wa idara mbambalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.   

Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema kwa lengo la kufanya tathimini ya Kampeni ya Chanjo ya Polio  kwa watoto walio chini ya umri wa  miaka 5 mitano pamoja  kupokea tathimini ya utekelezaji wa  zoezi la chanjo ya UVIKO 19 ambapo Manispaa ya Songea imefanikiwa kuchanja kwa asilimia 77% na kufikia lengo lililowekwa na Serikali la kuchanja  kwa 70%.

Pololet alibainisha kuwa zoezi la utoaji wa chanjo ya polio litatekelezwa kwa awamu nne ikiwa hadi hivi sasa Serikali imetoa chanjo ya Polio awamu tatu  hivyo bado awamu moja ili kukamilisha zoezi hilo, hivyo amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kukamilisha dozi za chanjo hiyo ili kuepukana na ugonjwa wa kupooza.

Alisema Utekelezaji wa zoezi la Chanjo ya Polio umetokana na baaada ya kugundulika kwa mgonjwa mmoja kutoka Nchi jirani ya Malawi na Msumbiji hivyo amewarai wananchi wote  kupeleka watoto wao kupata chanjo ya Polio  ya awamu ya nne ili  kutengeneza kizazi chenye afya njema.   


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa  zoezi hilo, Mratibu wa Huduma za Chanjo Manispaa ya Songea Moh’d Ally Khamisi alisema Manispaa ya Songea imetoa chanjo ya Polio kwa mitaa yote 95 ambapo awamu ya kwanza watoto lengwa walikuwa 32,962 waliochanjwani 41,552  sawa na asilimia 114%, pia awamu ya pili watoto lengwa ni 32,962  waliochanjwa ni  47,456  sawa na asilimia 142%, na awamu ya tatu watoto lengwa ni 44,962 waliochanjwa ni 59403 sawa na asilimia 132.1%.

Moh’d alibainisha kuwa ugonjwa wa Polio husababishwa na kirusi wa Polio ambao huingia mwilini kwa njia ya mdomo kutoka kwa mtu aliye na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Polio ambapo kinga yake ni matone ya Polio kwakuwa Kirusi haina matibabu.

Aliongeza kuwa ugonjwa huo huathiri sehemu ya mishipa, misuri, na wakati mwingine uti wa mgongo,na ubongo wa mtoto ambapo dalili zake hupatwa na maumivu ya kichwa, homa, kutapika, maumivu ya mgongo, misuri, na kukaza kwa misuri na kupata ulemavu.

Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuongeza kinga  dhidi ya ugonjwa wa kupooza kwa watoto kuanzia mwezi 0 hadi miezi 59 ndio waathirika wakubwa ukilinganisha na watu wazima.

Alisema “ Tusiogope chanjo yoyote itakayotokea bali tuogope  madhara yatakayoweza kujitokeza.”

IMEANDALIWA NA;

AMINA PILLY

AFISA HABARI.

                                                                                                                                  

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa