MANISPAA SONGEA YANUNUA MTAMBO WA KUZOLEA TAKA
Manispaa ya Songea imenunua mtambo wa kisasa wa kuzolea taka (kijiko ) ambacho kitaalam unafahamika kwa jina la back hoe loader.
Mtambo huo uliogharimu zaidi ya sh.milioni 170 umenunuliwa toka kampuni ya Hansom Tanzania Limited.
TEMESA imekagua mtambo huo na kuridhika kuwa mtambo huo ni wa kisasa ukiwa na vifaa muhimu vikiwemo kiyoyozi na muziki.
Tayari mtambo huo umeanza kazi ya ukusanyaji wa taka katika viunga vya Songea hivyo kupunguza muda wa kuzoa taka kwa kutumia nguvu kazi hali ambayo imesababisha mji wa Songea kuonekana wa kuvutia kutokana na kasi ya kuondoa taka ngumu.
Manispaa ya Songea inazalisha taka kiasi cha tani 71.5 kwa siku ambapo uwezo wa Manispaa hiyo kuzoa taka kwa siku ni kati ya tani 35 hadi 40 ambapo sasa manispaa inatarajia kuongeza uwezo wake wa kuzoa taka kwa siku.
Manispaa ya Songea yenye kata 21 na Mitaa 95 ina jumla ya wakazi 218,942 kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa