HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, imenunua makabati ya chuma (Cabinets ) 50 zenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa ajili maafisa watendaji wa Kata 21 na maafisa watendaji wa Mitaa 34.
Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa kwa watendaji hao, vimetokana na Fedha za mradi wa Uboreshaji wa Miji na Manispaa (ULGSP ) ambao unatekelezwa kwa fedha za serikali ikiwa ni mkopo toka Benki ya Dunia.Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 18 nchini zinazotekeleza mradi huo ambao una thamani ya zaidi ya sh.bilioni 21 .
Miradi mingine ambayo inatekelezwa katika mradi huo unaofanyika katika kipindi cha miaka mitano ni ujenzi wa barabara ya lami nzito zenye urefu wa kilometa 8.6, ukarabati wa Stendi ya Mabasi ya zamani, ununuzi wa magari mawili ya taka,ujenzi wa Stendi mpya ya mabasi ya Tanga,ujenzi wa machinjio, ukarabati wa bustani ya Manispaa na kujengea uwezo Halmashauri.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa