Na. Amina Pilly,
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mafanikio ya kupata hati safi kwa mara tano mfululizo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kanali Abbas ameagiza wakuu wa idara kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya majibu ya hoja pamoja na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG, akisisitiza umuhimu wa kutumia mifumo mipya ya ukaguzi na ufuatiliaji wa fedha. Vilevile, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi watakaobainika kusababisha hasara.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mheshimiwa Michael Mbano, amesema zipo hoja 35 zinazopaswa kujibiwa ndani ya siku 90, huku akieleza kuwa baadhi ni za kibajeti na kiutendaji zinazohitaji maelezo, uhakiki na kufungwa rasmi.
CAG Nicholaus Abnon Killinga amepongeza Halmashauri kwa kuvuka malengo ya mapato, akisema licha ya kupata hati safi, hoja 35 bado ni nyingi na zinahitaji mkakati madhubuti wa kuzifunga. Aliongeza kuwa matarajio ni kwamba Manispaa ya Songea itakusanya mapato makubwa zaidi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakili Bashir Muhoja, amesema hoja zilizohojiwa ni 36, ambapo hadi sasa 1 imefungwa, 27 ziko kwenye utekelezaji na 8 bado hazijatekelezwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Ruvuma, Komredi Oddo Mwisho, amepongeza uongozi wa Halmashauri kwa kusimamia maendeleo na huduma bora kwa wananchi, na kufanikisha ukusanyaji wa mapato kwa 100% kabla ya mwaka wa fedha kuisha
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa