HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepata Hati ya kuridhisha katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Tina Sekambo amesema Halmashauri hiyo imepata Hati ya kuridhisha kuanzia mwaka wa fedha wa 2015/2016,2016/2017 na 2017/2018.
Sekambo amebainisha mwenendo wa makusanyo kwa miaka mitatu mfululizo katika kipindi hicho cha miaka mitatu kuwa ni katika mwaka wa fedha wa 2015/2016,makisio yalikuwa ni kukusanya zaidi ya bilioni 3.247 ambapo makusanyo halisi yalikuwa ni zaidi ya bilioni 1.401 sawa na asilimia 43.
Amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017,makisio ya makusanyo katika Halmashauri ya Manispaa yalikuwa ni kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 3.135 ambapo makusanyo halisi yalikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 2.697 sawa na asilimia 86.
“Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018,makisio ya makusanyo kwa mwaka yalikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 3.349,ambapo makusanyo halisi yalikuwa ni zaidi ya bilioni 2.704 sawa na asilimia 81’’,amesema Sekambo.
Hata hivyo amesema hadi kufikia februari,2019 Halmashauri hiyo,imeweza kukusanya zaidi ya bilioni 1.720 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani ukiondoa mapato ya, vituo vya Afya na Ada za Shule.
Kulingana na Sekambo,hadi kufikia Februari, 2019 Halmashauri imepokea zaidi ya shilingi bilioni 21.736 sawa na asilimia 37 ya makisio ya bajeti ya Halmashauri.
Amesema kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 1.843 sawa na asilimia 58 ni makusanyo ya mapato ya ndani na zaidi ya shilingi bilioni 17.085 sawa na asilimia 62, ni fedha za mishahara.
Sekambo amesema zaidi ya shilingi milioni 678.72 sawa na asilimia 64 ni matumizi ya kawaida na zaidi ya shilingi bilioni 2.128 sawa na asilimia 8 ya mapokezi ya fedha za miradi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Katika mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi bilioni 59 kati ya fedha hizo na kwamba zaidi ya bilioni . 3.203 ni makadirio ya makusanyo ya mapato ya ndani,bilioni 27.751 ni Mishahara, zaidi ya bilioni 1,067 Matumizi ya kawaida(OC) na zaidi ya shilingi bilioni 27.220 ni miradi ya maendeleo .
Hata hivyo amesema hadi kufikia Februari,2019 Halmashauri imetumia zaidi ya bilioni 8.233 sawa na asilimia 14 ya makisio ya bajeti ya Halmashauri na kwamba kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 1.608 sawa na asilimia 87 ni makusanyo ya mapato ya ndani.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea, inaendelea kukusanya na kudhibiti ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielekroniki wa LGRCIS ambapo hadi sasa kuna mashine za ukusanyaji mapato (POS) 75.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa