HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imempata Naibu Meya Mpya Judith Mbogoro baada ya kushindwa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.Mbogoro ambaye alikuwa mgombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi alimshinda Mchungaji Martin Mlata mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.
Uchaguzi wa Naibu Meya ilikuwa ni moja ya ajenda katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea uliofanyika jana.Mbogoro amechukua nafasi ya aliyekuwa Naibu Meya Yobo Mapunda ambaye amemaliza muda wake.Katika uchaguzi huo jumla ya wapigakura 28 walipiga kura ,kura iliyoharibika ni moja. Katika matokeo hayo Mchungaji Martini Mrata alipata kura nne na Judith Mbogoro alipata kura 23.Katika mkutano huo pia aliapishwa Diwani mpya wa Viti maalum Ajira Rajabu Kalinga na kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wananchi wa Manispaa ya Songea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 3,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa