BARAZA la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limemchagua Asia Chikwale kuwa Naibu Meya mpya wa Manispaa ya songea.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Abdul Mshaweji ameongoza zoezi la uchaguzi wa Naibu Meya katika baraza la madiwani la mwaka wa fedha 2018/ 2019 ambalo limefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kikao hicho pia kimewashirikisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema pamoja na watumishi wa Idara na vitengo wa Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake, Mshaweji ameeleza umuhimu wa uchaguzi katika kulijenga taifa kwa kuwa kiongozi anayechaguliwa atashirikiana vyema na viongozi wa serikali na wananchi kuleta maendeleo ya Nchi.
“Uchaguzi huu unatija kwa wananchi naomba tuyatekeleze yote yaliyoainishwa.” Amesema Mshaweji
Naye, Diwani wa Viti Maalum aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Judith Mbogoro ametoa shukrani kwa madiwani wote na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Songea kwa ushirikiano aliupata katika kipindi chote alichokuwa Naibu Meya wa Manispaa na ameahidi kuwa atakuwa pamoja na kiongozi aliyechaguliwa na endapo atakwama sehemu atasita kumpa wazo.
“Najitambua na kujijua nitatoa ushirikiano daima.” Anasema Mbogoro
Vile vile, Diwani wa Viti maalum aliyechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Asiah Chikwale amesema kuwa nafasi aliyoipata ataitumia vizuri kwa kushirikiana na viongozi wengine kuleta maendeleo ya Manispaa ya Songea,Mkoa na Taifa kwa ujumla wake.
“ nimechaguliwa kwa ajili ya wananchi, nitawajibika kwa ajili yao.” Amesema Chikwale
Uchaguzi wa meya wa Manispaa unafanyika kila mwaka wa fedha Nchini Tnazania.
Imeandaliwa na
Farida Musa
Wa kitengo cha TEHAMA wa Manispaa ya Songea
September 5, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa