HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetenga eneo la upimaji wa viwanja lenye ukubwa wa ekari 172 katika Kata ya Lilambo kwa ajili ya viwanda.
Eneo hilo limepimwa kwa ajili ya viwanda vya kati na kwamba viwanja hivyo vitajumuisha matumizi mbaimbali kama ya huduma za kijamii,makazi na biashara,vituo vya mafuta,hoteli,soko,maeneo ya kuabudia na maeneo ya wazi.
Mradi huo wa upimaji wa viwanja katika Mtaa wa Lilambo B,ulianza kupitia mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Aprili 17,2018 ambapo jumla ya wananchi 317 walihudhuria na kupokea mradi huo.
Taratibu za kutoa ardhi kisheria zilifuatwa kulingana na sheria ya Ardhi namba nne yam waka 1999 ambayo inaeleza wazi kuwa ardhi yoyote inayotwaliwa na serikali,Taasisi au mtu binafsi ni lazima ilipwe fidia timilifu ambapo wananchi wote walikubali.
Jumla ya fidia yote kwa wananchi hao ni Zaidi ya shilingi milioni 233.84 zinahitajika kuwalipa wananchi 75 ambao ardhi yao imetwaliwa kwa ajili ya matumizi ya viwanda ni ekari 172.
Hata hivyo kutokana na fedha iliyotengwa awali ilikuwa ni shilingi milioni 54,ikijumuisha ulipaji wa fidia na upimaji,Idara ya ardhi imeandaa dokezo lenye wananchi 15 lenye thamani ya shilingi milioni 47.9 malipo ambayo yanatarajiwa kulipwa hivi karibuni
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 4,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa