• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MANISPAA ya Songea yapima viwanja zaidi ya 35,000

Tarehe ya kuwekwa: April 30th, 2019

HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ina jumla ya viwanja 35,500 vilivyopimwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Tina Sekambo amesema Kati ya hivyo viwanja 18,489 ramani zake zimesajiliwa na kwamba maeneo ambayo ramani zake hazijasajiliwa yameundiwa kamati Kwa kuwashirikisha Wananchi ili kukamilisha Upimaji kwa njia ya Upimaji shirikishi.

“Halmashauri imetekeleza agizo la serikali kwa kuhakikisha maeneo yote ya umma yanapimwa na kuandaliwa hati. Maeneo hayo yanajumuisha vituo vya afya, Maneo ya shule za Msingi na Sekondari, Zahanati pamoja na Ofisi za Umma’’,alisema.

 

Hata hivyo Sekambo amesema, hadi sasa jumla ya maeneo 170 yamepimwa na mengine yamepimwa kwa hatua ya awali (Demarcation) na mchakato wa kukamilisha upimaji huo unafanyika na ramani hizo zinasajiliwa.

Kulingana na Mkurugenzi huyo,Halmashauri ya Manispaa ya Songea,imeandaa Mpango kabambe (MasterPlan) ambao umeidhinishwa na Wizara na utatumika katika kipindi cha miaka 20 (2017-2037) kama dira ya maendeleo ya Mji wa Songea.

 

Amesema Katika mpango huo, Halmashuri imetenga matumizi mbalimbali ambayo yataleta tija katika Mji wa Songea ikiwemo maeneo ya viwanda katika kata ya Lilambo, Mletele, Tanga na Eneo la Uwekezaji EPZA Mwengemshindo lenye jumla ya hekari 5000.

Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo imetenga na kupima eneo la ekari 170 lililopo katika Kata ya Lilambo kwa matumizi ya Viwanda.

Kuhusu makisio ya ukusanyaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2018/2019,Sekambo amesema Manispaa ya Songea ilipangiwa kukusanya jumla ya sh.milioni 600 ambapo hadi sasa zimekusanywa sh.milioni 316 toka  kwa wamiliki wa viwanja mbalimbali na kwamba wananchi 274 wamefikishwa Mahakamani kwa kukaidi kulipa kodi ya pango la ardhi.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea

Aprili 30,2019

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa