MANISPAA ya Songea Mkoa wa Ruvuma, imempoteza Diwani wa CCM Mariam Yusuph ambaye alifariki Dunia kwa ajali ya gari Novemba 30 mwaka huu.
Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Lumecha wilayani Songea.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushy marehemu akiwa na wenzake walikuwa wanatoka wilayani Tunduru kwenye uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Ruvuma.
Marehemu tayari amezikwa nyumbani kwao mkoani Iringa. Madiwani wa Manispaa ya Songea na wakuu wa Idara na Vitengo hawataweza kumsahau Mariam kutokana na uchapakazi wake na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Songea.
Angalia video hii wakati Mariam wakati wa uhai wake akiwa na Kamati ya Fedha na Uongozi anahoji mradi wa maji uliogharimu sh milioni 517 katika Mtaa wa Mitendewawa kata ya Chandarua .ilikuwa ni Oktoba 26 mwaka huu.
Manispaa ya Songea mwezi Novemba pekee imepata pigo kubwa kwa kuwa imempoteza aliyekuwa Mbunge wake Leonidas Gama na sasa Aliyekuwa Diwani wake Mariam Yusuph.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa