IDARA ya maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya mpango wa maendeleo ya sekta ya maji awamu ya kwanza (WSDP I) ambapo Halmashauri ilitekeleza miradi katika mitaa tisa kwa asilimia 100 iliyogharimu jumla ya Tshs. 1,656,786,632/.
Mkuu wa Idara ya Maji katika Manispaa hiyo,Mhandisi Samwel Sanya amesema,miradi ya Mitendewawa na Luhilakati imekamilika kwa asilimia zaidi ya 80 ambapo watu 4141 wanapata huduma.Amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika bajeti yake ilipanga kujenga miradi ya visima vya maji 90 katika mitaa 15 ambapo hadi sasa miradi katika mitaa hiyo ipo katika hatua tofauti tofauti ya utekelezaji itakayo hudumia wananchi 22,500.
Mhandisi Sanya amebainisha zaidi kuwa,Katika mwaka wa fedha 2017/2018 zimepokelewa jumla ya Tshs. 485,387,405.00 na kwamba hadi kufikia Juni 2018 jumla ya Tshs.389,811,424.00 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika mitaa ya Mitendewawa na Ruhilakati.
Takwimu zinaonesha kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni asilimia 46.6
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 19,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa