HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma katika mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga Tshs 169,768,620.00 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake 100 na vijana 77. Hadi kufikia Juni, 2018 jumla ya Tshs 196,000,000.00 sawa na asilimia 115 zimetolewa na kukopeshwa kwa vikundi 154 kati ya hivyo vikundi vya Wanawake 127 vimekopeshwa Tshs. 162,100,000.00 na vikundi vya vijana 27 vimekopeshwa Tshs 33,900,000.00.
Mikopo hiyo ililenga katika kila kikundi kuendeleza mradi waliokuwa wameuanzisha hivyo kutengeneza ajira kwa vijana na akina mama.Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilitenga Tshs 174,000,000 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake na vijana 70.
Hadi kufikia Juni 2017 Halmashauri ilikopesha jumla ya Tshs. 88,800,000.00 sawa na asilimia 51 kwa vikundi 133 kati ya hivyo vikundi vya Wanawake 77 vilikopeshwa Tshs. 59,800,000.00 na vikundi vya Vijana 56 vilikopeshwa Tshs. 29,000,000.00.
Kuhusu Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia TASAF awamu ya III, ulianza kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia kipindi cha mwaka wa fedha cha 2015/2016, jumla ya mitaa 53 imenufaika na mpango na idadi ya kaya zilizofikiwa ni 4,878.
Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 4,044,549,300.00 kwa ajili ya kuwalipa walengwa 4,878 sawa na asilimia 100 ya walengwa wote hadi kufikia mwezi Juni 2018 kwa lengo la kusaidia kaya masikini kujikimu kiuchumi.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 20,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa