MANISPAA ya Songea kupitia Idara ya Mifugo na uvuvi imeanza kutoa elimu kabla kuwaondoa wafanyabiashara wote ambao wanauza samaki katika maeneo ambayo hayapo kisheria hali ambayo inachangia kuikosesha mapato Manispaa hiyo.
Idara ya Mifugo na uvuvi imezunguka katika viunga vya Manispaa ya Songea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wanauza samaki na dagaa maeneo ambayo sio soko likiwemo eneo la nje ya stendi ya Mfaranyaki ambako kuna akinamama wengi wanafanya biashara hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na uvuvi Rozina Chuwa amesema biashara ya samaki na dagaa inatakiwa kufanyika kwenye masoko ya Manzese na Lizaboni .Amesema kufanya biashara ya samaki na dagaa nje ya soko ni kosa ambapo ukikamatwa unaweza kupigwa faini ya kuanzia shilingi 200,0000.
Chuwa àmesema kuanzia sasa hairuhusiwi kusafirisha magunia ya dagaa kwenye basi na kwamba Mfanyabiashara biashara yeyote anayetaka kusafirisha mzigo wa dagaa au samaki anatakiwa kutumia magari ya mizigo na kwamba ni lazima àpate kibali cha kusafirishia ambacho kinatolewa bure na Manispaa ya Songea.
Wafanyabiashara hao wameipongeza Manispaa kwa elimu ambayo wameipata ambapo wameahidi kuondoka na kwenda katika maeneo rasmi ya masoko.
Sheria ndogo ndogo ya Manispaa ya Songea ya mwaka 2010 inawataka wafanyabiashara wa samaki wa jumla na rejareja kuuaza samaki zao katika maeneo maalum ya masoko na sheria mama ya uvuvi ya mwaka 2009 zinawataka wafanyabiashara wa samaki kukata leseni na kuwa na vibali halali.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa