NAIBU Meya wa Manispaa ya Songea Yobo Mapunda amesema Mkataba wa matengenezo ya barabara za lami nzito zenye urefu wa kilometa 10.3 umesainiwa na Mkandarasi Kampuni ya Kichina tayari ipo Songea kuanza kazi hiyo mwezi huu ambayo itachukua miezi 18 na kugharimu zaidi ya bilioni kumi.
Manispaa ya Songea ilivunja mkataba na Mkandarasi wa kwanza Kampuni ya Lukolo baada ya kushindwa kumaliza kazi ndani ya mkataba.Mapunda alikuwa anazungumza na wananchi wa kata ya mjini Manispaa ya Songea katika ziara ya Mbunge wa jimbo la songea mjini DK Damas Ndumbaro ambaye anapita katika kata zote 21 kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa Mbunge wao sanjari na kusikiliza kero za wananchi.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa