• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mazishi ya Muasisi wa TANU Alhaji Mustapha Songambele

Tarehe ya kuwekwa: June 3rd, 2025

Songea, Ruvuma – Juni 2, 2025:
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndugu Emmanuel John Nchimbi, ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Muasisi wa Chama cha TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika, Hayati Alhaji Mustafa Mohammed Songambele, yaliyofanyika katika Kijiji cha Bombambili, Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Hayati Songambele alifariki dunia tarehe 1 Juni 2025 akiwa na umri wa miaka 100, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Marehemu alizaliwa tarehe 25 Mei 1925 na aliadhimisha karne moja ya maisha yake tarehe 25 Mei 2025.

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu Nchimbi alisema:

“Chama cha Mapinduzi na Serikali vimepata msiba mkubwa. Tumempoteza mmoja wa waasisi mashuhuri wa TANU, mzalendo na shujaa wa uhuru wa taifa letu. Mzee Songambele ametuachia hazina kubwa ya historia ya nchi kupitia kitabu alichoandaa kiitwacho Safari ya Karne. Chama kitadhamini na kusimamia kukamilika kwa kitabu hiki ili Watanzania wapate kujifunza kutoka maisha yake.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed, aliwasilisha salamu za pole kwa familia ya marehemu na kusema:

“Tumempoteza kiongozi mwenye busara, aliyekuwa tayari siku zote kutoa ushauri na hekima kwa vizazi vya sasa. Ni jukumu letu kuendeleza misingi ya haki, utu na uzalendo aliyoisimamia.”

Wasifu wa marehemu ulisomwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo, ambapo ilielezwa kuwa Hayati Songambele alikuwa Mkuu wa Wilaya ya kwanza wa Ilala baada ya uhuru mwaka 1961, na pia alihudumu kama Mkuu wa Mikoa ya Pwani (sasa Dar es Salaam) na Shinyanga. Pamoja na kuwa muasisi wa TANU, alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Hayati Songambele ameacha wake watatu, watoto 27 na wajukuu 74. Amezikwa kijijini kwao Bombambili kwa heshima za kitaifa na kwa uwepo wa viongozi mbalimbali wa serikali, chama na wananchi wa Ruvuma.

Mwisho

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Chupa 14,789 za Damu Kukusanywa Mkoani Ruvuma

    June 04, 2025
  • Mazishi ya Muasisi wa TANU Alhaji Mustapha Songambele

    June 03, 2025
  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • Tazama zote

Video

katibu Mkuu CCM Taifa Aongoza Maziko ya Alhaji Songambele
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa