Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka 2023 imepitia miradi 10 yenye thamini ya shilingi 2,727,619,229.18 kati ya fedha hizo michango ya wananchi shilingi 2,000,000.00, Serikali Kuu shilingi 1,447,715,329.18, Wadau/Wahisani/Mtu binafsi wa maendeleo shilingi 1,264,903,900.00 na Halmashauri ni shilingi 13,000,000.00 ambapo kati ya hiyo 4 imefunguliwa, 1 umezinduliwa, 1 ni ugawaji wa vyandarua na 4 imetembelewa.
Ndugu Abdalla Shaibu Kaim Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amezitaka Halmashauri zote Nchini zihakikishe zinaandaa miche ya miti zaidi ya 500 ambayo itapandwa ili kulinda na kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa lengo la kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanatunzwa na kusimamiwa vizuri kwa ustawi wa viumbe hai na Taifa kwa ujumla.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023; “MABADILIKO YA TABIA NCHI, HIFADHI YA MAZINGIRA NA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI, chini ya kauli Mbiu; Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa’’.
Imeandaliwa;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa