MBUNGE ASHAURI MANISPAA IWE NA KITUO CHA UTALII
MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini Leonidas Gama ameshauri wakati Bustani ya Manispaa ya Songea inaelekea kukamilika,ameshauri bustani hiyo pia iwe na kituo cha kutoa taarifa za utalii.
Amesema mkoa wa Ruvuma hauna vituo vya kutoa taarifa za utalii(Tourism Information Centre) hivyo bustani hiyo ikiwekwa huduma ya kutoa taarifa za utalii inaweza kuvutia idadi kubwa ya watalii na wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza katika Manispaa ya Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepokea jumla ya sh.milioni 400 kwa ajili ya uboreshaji wa Bustani ya Manispaa ya Songea.
Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa Kuzijengea uwezo serikali za mitaa(ULGSP) unatarajiwa kugharimu sh.milioni 399.95.
Fedha ambazo zimelipwa hadi sasa ni sh.milioni 97.83 na fedha ilibaki ni sh.milioni 302.12.Mradi huo unaofanyika kwa miezi sita ulianza Machi 15 mwaka huu na unatarajiwa kumalizika Septemba 30,2017.
Mradi huo uliopo mkabala ya Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Songea una eneo la mgahawa,choo cha kulipia,uzio na maeneo ya kupaki magari(parking bay).
Bustani hiyo ya aina yake katika mji wa Songea ina eneo la kupumzikia(resting huts) na kwamba hatua ya ujenzi imefikia zaidi ya asilimia 80.
Maeneo mengine ambayo yanaendelea katika bustani hiyo ni ujenzi wa uzio kuzunguka bustani yote,utengenezaji wa bustani ambayo inawekwa udongo na kupandwa nyasi na miti na ujenzi wa mnara na kazi ya kusambaza maji katika eneo la ujenzi.
Manispaa ya Songea ni moja ya Halmashauri za miji na Manispaa 18 za Tanzania Bara ambazo zipo katika mpango wa ULGSP lengo likiwa ni kuendeleza miundombinu yake.
Halmashauri nyingine ni Sumbawanga, Singida, Tabora, Shinyanga,Musoma,Moshi,Lindi, Morogoro, Iringa, Babati, Msasi, Kibaha, Njombe, Mpanda,Korogwe na Geita.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa