Na; Amina Pilly
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini leo juni 27 imekabidhi kompyuta sita zenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, sambamba na kufanya ukarabati wa Kituo Kikuu cha Polisi Songea pamoja na Kituo cha Polisi Lizaboni.
Akikabidhi kompyuta hizo ndugu Juma Mpeli amesema kwa niaba ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini alisema, lengo la kutoa vifaa hivyo ni kusaidia taasisi zilizopo katika Jimbo la Songea kutekeleza majukumu yake kiufanisi ikiwemo Jeshi la Polisi.
“tunaamini kupitia vifaa hivi na ukarabati unaoendelea utasaidia kuboresha hali ya Ofisi za Polisi katika kuhudumia wananchi wa Jimbo hili la Songea Mjini ambalo yeye ndiyo mwakilishi wake” Alisema Mpeli.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songea (OCD), Kilangi Kabisi, amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini kwa msaada wa kompyuta hizo, akieleza kuwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu ya kila siku, kutunza kumbukumbu muhimu, na kurahisisha utoaji wa taarifa kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Polisi Lizaboni, Steven Mlaponi, amepongeza jitihada za Mbunge kwa kuonesha ushirikiano mkubwa katika kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Lizaboni, hatua inayolenga kuboresha huduma za kiusalama kwa wananchi wa eneo hilo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa