Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
21 MACHI 2022
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro (MB) ametoa Mazulia 180 kwa Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Ruvuma kwa ajili kupunguza changamoto ya upungufu wa mazulia katika misikiti hiyo.
Msaada huo umetolewa hapo jana tarehe 20.03. 2022 katika viwanja vya Msikiti wa Wilaya uliopo ndani ya Manispaa ya Songea.
Akizungumza wakati akikabidhi mazulia hayo kwa viongozi wa Jumuiya ya wanawake wa kiislamu Manispa ya Songea, alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kupunguza changamoto iliyopo ya upungufu wa vifaa vya kuswalia katika maeneo hayo ya nyumba za ibada.
Alisema kuwa mazulia hayo yatagawika kwa misikiti 8 ambapo kila msikiti utapata mazulia 22 ambayo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na Jumuiya hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali katika nyumba za ibada hususani misikiti.
MWISHO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa