NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
01.11.2021
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imezindua rasmi miradi ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu kwa lengo la kuanza utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu hiyo.
Miradi hiyo ilizinduliwa na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro iliyofanyika katika kata ya Subira Manispaa ya Songea 31 Oktoba 2021 ambayo ilihusisha ujenzi wa madarasa mawili pamoja na mradi wa maji utakaojengwa katika Kata hiyo pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika Bwalo la chakula katika Sekondari ya Emanuel Nchimbi.
Dkt. Ndumbaro alisema kuwa fedha hizo zilizotolewa haziwezi kutatua changamoto zote zilizopo na hivyo amewataka wananchi kuchangia nguvu zao ili kuokoa kiasi cha fedha ili ziweze kuongeza mradi mwingine. Ikumbumbukwe ya kuwa Manispaa ya Songea imepokea fedha million 660,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Sekondari 26, ujenzi madarasa katika vituo shikizi kwa shule za msingi Nonganonga pamoja na ujenzi wa bwalo la chakula kwa shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalmu katika shule ya Msingi Ruhila.
Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea imejipanga kujenga mradi wa gofu ambao utasaidia kujenga hoteli kubwa 5 na kuongeza fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta maendeleo na kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara kama ilivyo kwa mji mitano pekee nchini Tanzania yenye viwanja vya gofu ambayo ni Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro na Mufindi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kusimamia wahandisi wote kwa kuhakikisha wanakuwepo kwenye maeneo ya ujenzi wa miradi ili waweze kusimamia kwa ufanisi na kwa uhakika wa ubora wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Kamando amesisitiza kuwa miradi hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa wakati ambapo hadi kufikia tarehe 15 Disemba 2021 miradi hiyo itakabidhiwa rasmi kwenye tathimini ya Mkoa wa Ruvuma na hivyo wataalamu wahakikishe wanakuwa makini katika kusimamia zoezi hilo.
Amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kufanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yao ili kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuhakikisha maeneo yaliyochaguliwa kujenga miradi hiyo hayabadilishwi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Hamisi Abdallah Ally amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa madarasa hayo ili kufanikisha ujenzi huo.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na kupanda kwa bei ya mbolea alisema kuwa tatizo la kupanda kwa bei ya mbolea imetokana na kufungwa kwa viwanda vya kuzalisha mbolea kutoka nchi za nje zilizoendelea kutokana na ugonjwa wa UVIKO 19.” alibainisha”
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa UVIKO 19 pamoja na kuendelea kupata chanjo kwa hiari ya ugonjwa huo.
Mwisho.
.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa