Na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI
MANISPAA YA SONGEA.
Waziri wa Maliasili na Utalii DKT. Damasi Ndumbaro Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, leo tarehe 18 oktoba 2021 amegawa mifuko ya Saruji 40 fedha kutoka Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa moja Shule ya Msingi Nonganonga iliyopo Kata ya Mletele Manispaa ya Somgea.
Akiongea kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, katibu wa Mbunge Ndugu Joel Ndunguru amesema changamoto hiyo ilibainika wakiwa katika ziara ya kamati ya Siasa Wilaya ambapo kupitia ofisi ya Mbunge iliahidi kusaidia saruji ili kuunga mkono jitihada za wananchi ambao waliweza kuchangia nguvu kazi za kujenga darasa hilo na kisha kuezekwa fedha kutoka kwa Mkurugenzi Manispaa ya songea.
Aliongeza kuwa katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi DKT.Ndumbaro (MB) ametoa fedha milioni 20,000,000/= kwa ajili ya ukamilishaji wa Bwalo la chakula katika Sekondari ya Emmanuel Nchimbi ambalo lipo hatua ya ukamilishaji.
Naye Diwani wa kata ya Mletele Gerard Maurus Lungu ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini kwa Msaada uliotolewa ambao utasaidia kukamilisha darasa moja ambalo litasaidia kupunguza sehemu ya changamoto za miundombinu zinazoikabili shule hiyo.
MWISHO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa