• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Meya Mbano; Amewataka Wananchi Kulinda Haki za Watoto

Tarehe ya kuwekwa: June 16th, 2025

Na; AMINA PILLY

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mheshimiwa Michael Mbano, leo tarehe 16 Juni 2025, ameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kata ya Mfaranyaki, Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Katika hotuba yake, Mhe. Mbano amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira bora kwa watoto kwa kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi kidato cha sita, pamoja na kuboresha upatikanaji wa chanjo na huduma bora za afya. Aidha, amesema serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kupambana na ndoa za utotoni na ajira za watoto.

Hata hivyo, Meya Mbano ametaja kuwepo kwa changamoto zinazowakumba watoto, hasa wale wa mitaani ambao hukosa fursa ya kupata elimu kutokana na umasikini na kukumbwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuwa mustakabali wa mtoto wa Afrika ni wenye tumaini. Hii inahitaji kuwekeza zaidi katika elimu bora na jumuishi, huduma za afya kwa watoto hususani vijijini, ulinzi dhidi ya ukatili wa aina zote, pamoja na ushiriki wa watoto katika maamuzi yanayowahusu,” alisema Mheshimiwa Mbano.

Aidha, ametoa wito kwa jamii, wazazi na walezi kuwalea watoto kwa maadili mema, kuwalinda, na kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake, akisoma risala kwa niaba ya watoto mbele ya mgeni rasmi, Happiness Mbunda ameiomba Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuimarisha ulinzi wa mtoto. Alisisitiza kuwa taifa imara hujengwa kwa kuwekeza katika maendeleo ya watoto wake.

Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Juni, kwa kumbukizi ya mauaji ya watoto wa Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976 waliouawa walipokuwa wakipigania haki yao ya kupata elimu bora.

Mwisho

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Meya Mbano; Amewataka Wananchi Kulinda Haki za Watoto

    June 16, 2025
  • Meya wa Songea Atoa Wito kwa Familia Kuchangia Damu Kuokoa Maisha.

    June 14, 2025
  • Manispaa ya Songea Yapata Hati Safi kwa Miaka 5 Mfululizo.

    June 13, 2025
  • Wasira Amewataka Wananchi Kulinda Amani ya Taifa.

    June 13, 2025
  • Tazama zote

Video

SONGEA MC YAPATA HATI SAFI KWA MIAKA 5 MFULULIZO
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa