Mnyama huyu adimu duniani anaweza kufungua milango ya utalii katika ukanda wa kusini kwa sababu wanyama hao wamesalia wachache na wapo katika hatari ya kutoweka kusini mwa Tanzania.
Hifadhi na misitu michache nchini ambayo Mbega weupe wanapatikana ndiyo maana katika ukanda wa kusini ni Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma wanyama hawa adimu wanapatikana.
Wanyama aina ya mbega weupe katika ukanda wa kusini wanaopatikana katika msitu wa Liwilikitesa Wilaya Mbinga Mkoa Ruvuma wapo katika hatari ya kutoweka baada ya kushambuliwa na wawindaji haramu.Hata hivyo katika kanda ya kaskazini Hifadhi ya Taifa ya Arusha wanapatikana kwa wingi wanyama aina ya mbega weupe ambao wanavutia idadi kubwa ya watalii.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa