MGUNDUZI wa madini ya Tanzanite katika eneo la Mirerani mkoani Manyara, Mzee Jummane Ngoma amesafirishwa kwenda nchini India kupatiwa matibabu.Mzee Ngoma baada ya kutambuliwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli alipewa kupewa Shilingi Milioni 100.
Rais Magufuli alitoa kiasi hicho cha pesa April 2018 wakati alipozindua Ukuta wa Mirerani ambapo alisema ugunduzi wa Mzee Ngoma ndio umeiweka Tanzania katika ramani ya madini hayo.
Kwa mujibu wa mtoto wake, Mzee Ngoma amesafirishwa Jumatatu Julai16,2018 kwenda katika hospital ya Apollo nchini India.Mzee Ngoma amepelekwa nchini humo kwa sababu anasumbuliwa na maradhi ya kupooza.
Mzee Ngoma aliyezaliwa mwaka 1939, aligundua madini ya Tanzanite mwaka 1967.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa