Na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA
18 Desemba 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Selemani Jafo amewataka wananchi na viongozi kupanda miti million 276 kwa Nchi nzima, kwa jumla ya Halmashauri 184 na kila Halmashauri inapaswa kupanda miti Millioni 1.5 kila mwaka.
Hayo yametamkwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Selemani Jafo akiwa ziarani Mkoani Ruvuma iliyofanyika leo tarehe 18 mwezi desemba 2021 na kufanikiwa kutembelea mradi wa Machinjio ya kisasa na chanzo cha maji kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la kukagua maendeleo halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Mheshimiwa Jafo alianza kwa kuwapongeza Wataalamu na viongozi wote kwa usimamizi bora wa mradi wa Machinjio mpya ya kisasa yenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300 kwa siku ambapo kwa kwasasa machinjio hiyo imeanza kufanya kazi ya uchinjaji wang’ombe 40 kwa siku.
Akizungumzia suala la utunzaji wa Mazingira alisema“ agenda za mazingira ni agenda muhimu sana bila kudhibiti uhalibifu wamazingira Nchi yetu itaendelea kuwa katika janga kubwa sana, hivyo amewataka viongozi kuongeza umadhubuti wa kusimamia na kuweka misingi mizuri ili uhalibifu uweze kukomeshwa”. “Mh. Jafo alisisitiza”
Aliongeza kuwa hivi karibuni katika Nchi yetu imejikuta imeingia katika changamoto kubwa ya ukosefu wa maji na umeme hususani katika maeneo ya vijijini, ambapo changamoto ya umeme imeonekana kuwa vyanzo vya maji ambavyo umeme wa maji ulikuwa ukitumia nishati kupitia maeneo mengi sana mabwawa yameendelea kushuka chini ya kiwango ambapo hupelekea kuwepo kwa mgao mkubwa wa umeme.
Alisema baadhi ya maeneo mengi ya mekutwa na changamoto ya maji hususani maeneo ya vijijini ambapo imetokea mifugo kukosa malisho bora na maji ambayo husababisha baadhi ya wanyama hao kufa. Hivyo amewataka wananchi kuachana na Imani potofu ya kushindana kuchoma misitu ovyo kwa dhana ya kudhani moto ukiuwasha na ukifika mbali utaishi maisha marefu duniani.
Ametoa rai kwa viongozi wote Mkoani Ruvuma kufuata sheria sura namba 20 ya mwaka 2004 ya ambayo inakutaka kuacha kuzingatia mita 60 sitini, pia kwa wale wote watakao bainika wanavunja sheria hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Naye kaimu Afisa Mazingira Mkoa wa Ruvuma Deogratius Sibula alisema Mkoa wa Ruvuma umekuwa ukiratibu mambo mbalimbali ya usimamizi wa sera na usimamizi wa mazingira ikiwemo na shughuli za usafi wamazingira, uhifadhi kwa lengo la kuyafanya mazingira yawe katika hali ya usalama ili kuboresha afya za binadamu na ustawi wa viumbe hai.
Sibula alisema Uzalishaji wa taka Mkoani Ruvuma katika Wilaya zote ni jumla ya tani 39,596,000 kwa mwaka ambapo sehemu kubwa ya taka ni za majumbani, viwandani na sokoni ambapo asilimia kubwa ya taka hizo hudhibitiwa kupitia mashimo ya taka kwa kuteketezwa kwa moto, ikiwa Manispaa ya Songea huzalisha taka ngumu tani 71.5 kwa siku
Aliongeza kuwa Halmashauri zinaendelea kutenga eneo la dampo ikiwemo na Halmshauri ya Manispaa ya Songea inayo eneo lenye mita za mraba 29.3 lililopo kata ya Subira mtaa wa Muungano ambalo limeandaliwa mwaka 2008 na tayari limeshapimwa.
Naye Eng. Francisco Mapunda Mhandisi wa Maji SOWASA alisema Mfumo wa maji safi SOWASA una vyanzo 9 ikiwemo na mlima wa matogoro, Lipasi, Luhira B, Luhira A, Mahilo, zenye uwezo wa uzalizashaji wa Lita Million 11,500,000 wakati wa masika na lita Million 1.438,000 wakati wa kiangazi huku mahitaji halisi Manispaa ya Songea ni lita Million 17,897,000.
Eng. Mapunda aliongeza kuwa vyanzo vyote hivyo maji yake hutibiwa na kuchujwa katika mitambo ya maji safi iliyopo Matogoro yenye uwezo wakutibu maji lita Milion 11,500,000 kwa siku.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa