Na;
AMINA PILLY
AFISA HABARI.
17 Agosti 2022
Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mjini Methew Ngalimanayo amewataka wananchi wa kata ya Mjini Manispaa ya Songea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa pamoja na kushiriki kuhesabiwa siku ya Sensa itakayofanyika tarehe 23 agosti 2022 ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi kwa lengo la maendeleo ya Taifa letu.
Hayo yametamkwa kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya Mjini uliofanyika jana tarehe 16 agosti 2022 katika viwanja vya Soko Kuu Songea Mjini ulioshirikisha viongozi wa dini, vyama vya siasa Wilaya/kata, wataalamu na vikundi mbalimbali vya ngoma kwa ajili ya kutoa elimu ya Sensa kwa wananchi wa kata hiyo.
Ngalimanayo alibainisha kuwa Sensa ilianzishwa mara baada ya nchi mbili kuungana 1964 (Tanganyika na Zanzibar), na baada ya kuungana mataifa yote mawili, mwaka 1967 ilifanyika Sensa ya kwanza Tanzania kwa lengo la Serikali kupata takwimu za wananchi ili kupanga maendeleo.
Alisema Serikali huandaa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu jinsia, watu wenye makundi maalum kama walemavu, watoto, elimu ambapo endapo mwananchi hatatoa taarifa ushirikiano kwa karani wa Sensa serikali haitaweza kupata takwimu sahihi.
Miongoni mwa taarifa zitakazo ulizwa na karani wa Sensa ni pamoja na umri, hali ya ndoa, jinsi, shughuli za kiuchumi, hali ya uzazi, vifo vitokanavyo na uzazi, kilimo, mifugo, uvuvi, misitu, majengo/nyumba na nyinginezo.
Naye mwenyekiti wa CCM Songea Mjini Hamisi Abdallah Ally amewataka wananchi wa kata ya Mjini kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Diwani za kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa na kukubali kuhesabiwa ili kupata idadi kamili ya Mtaa, kata na Taifa kwa ujumla.
Naye kiongozi wa dini ya kiislamu alisema “Mtume Mohamad (S.W) alihesabiwa Sensa” alisema Sensa ya Watu na makazi imetamkwa hata katika vitabu vya mungu kwasababu imeeleza kuwa waliteuliwa mitume 25 kwa ajili ya kufanya kazi ya dini katika maeneo mbalimbali kwa maana hiyo ni Sensa. Hivyo amewataka waislamu wote kufahamu kuwa Sensa ipo hata katika maandiko ya mungu.
Naye kiongozi wa dini ya kikristo alisema “Sensa ya mbinguni kuna wenye uhai wanne, wazee wanne wanao kizunguka kiti cha enzi wakitamka neon Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu kwa wakati wa usiku na mchana, wazee 24 katika kiti cha enzi cha yehova ambao wanawakilisha uumbaji wa Mungu, kuna nyota na mwezi ambazo Mungu anafahamu idadi yake.”
Aliongeza kuwa, Yesu alionesha utoshelevu wake kwakulisha wanaume 5000 kwa mikate mitano na samaki mawili wakawalisha wanaume 5000 bila kuhesabu wanawake na watoto, pia alionyesha kuwa nawanafunzi 12 kamati kuu watu ya watatu, kwahiyo Sensa imeendelea kufanyika toka agano la kale adi jipya.
Wananchi kwa nyakati tofauti walisema wapo tayari kuhesabiwa siku ya Sensa tarehe 23 agosti 2022.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa