Na; Amina Pilly.
Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Afya, amekuwa Serikali ya awamu ya sita imejipanga kikamilifu katika kupambana na maambukizi mapya kwa kutoa chanjo bure ya homa ya INI aina ya B kwa watoto wachanga na walio chini ya miaka mitano (5), pia kwa watu wazima kwa gharama nafuu kupitia vituo vya afya sambamba na utoaji wa elimu na upimaji wa mara kwa mara.
Tamko hilo limetolewa siku ya maadhimisho ya siku ya Homa ya INI Duniani iliyofanyika tarehe 28 Julai 2025 Mkoani Ruvuma katika Ukumbi wa Songea Club ambayo yalihusisha viongozi mbalimbali ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya,Halmashauri na wadau.
Alisema “ Katika kuelekea kutokomeza Homa ya INI ifikapo 2030 kama ilivyowekwa kwenye shirika la afya Duniani (WHO) serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesema itaendelea kutoa huduma za matibabu bure kwa wagonjwa wa homa ya INI nchini.
Aliongeza kuwa, Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022/2023, kiwango cha maambukizi ya homa ya INI aina ya B imeshuka kutoka 4% mwaka 2026/2017 hadi 3.5% ambapo mafanikio hayo yanaonesha kuwa vita dhidi ya ugonjwa huu unaoendelea kuzaa m,atunda, ambapo shirika la Afya Duniani WHO inakadiria kuwa na watu Mil. 254 wanaishi na homa ya INI aina ya B Duniani, pia zaidi ya Mil. 1.1 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huo. “Alisema.”
Akizungumnza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed alisema watu 24,000 wameathika na homa ya INI kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa uliofanyika mwaka 2022/2023 kiwango cha maambukizi ya homa ya INI wenye umri wa miaka 15 ni asilimia 2.0 sawa na watu wawili katika kila watu 100 wakiwemo wanaumeme 17,000 na wanawake 7000.
Kanali Ahmed alianza kwa kupongeza Serikali ya wamu ya sita kwa kazi nzuri inayofanywa ambapo Mkoa wa Ruvuma umepokea vifaa tiba,imepata miundombinu ya kisasa, pamoja huduma ya madaktari bingwa. “ Alisema”
Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusu vyanzo hatarishi vya maambukizi ya homa ya INI ili kuongeza kasi na kupunguza maambukizi mapya yatokanayo na ugonjwa huo.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa