Mstahiki Meya Manispaa ya Songea mheshimiwa Michael Mbano amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa Manispaa ya Songea wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa zoezi la usafi wa Mazingira.
Mhe. Mbano ametoa agizo hilo kupitia kwenye kikao cha baraza la kazi la Madiwani lililofanyika leo tarehe 30 Julai 2024 kwa lengo la kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata kuelekea siku ya Mkutano wa Baraza la Madiwani ambalo linatarajia kufanyika kesho tarehe 31 Julai 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea saa 4:00 asubuhi.
Alisema “ Mji ni mchafu hivyo kila Mtendaji wa Kata/Mtaa atekeleze wajibu wake na uwekwe Mkakati wakuhakikisha zoezi hilo linafanyika kisha itolewe taarifa ya utekelezaji wa maelekezo hayo, pia amewataka watendaji hao kutumia sheria ndogo za usafi wa mazingira.” Amesisitiza.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa