Afisa michezo Manispaa ya Songea Mohamed Kitesi amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujifunza kutengeneza mpango wakuweka akiba ambayo itaweza kuwasaidia wakati wa sasa na wa baadae, lililofanyika kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kuanzia 12-14/08/2020.
Kitesi amesema kongamano hilo limeshirikisha Wavuvi, Wakulima, Wajasiliamali wadogo wadogo, Madereva Bajaji, pamoja na Wanafunzi wa Sekondari zilizopo manipsaa ya Songea.
Majimaji Selebuka huendesha shughuli zake chini ya taasisi Songea Mississippi Foundation iliyopo Manispaa ya Songea, ambao katika kongamano hilo wameshirikisha wadhamini NMB, NHIF, LATRA kwa lengo kuu kutoa elimu ya ujasiliamali kwa madereva bajaji, wakulima, na wajasiliamali wadogo pamoja na kuibua vipaji vya michezo mbalimbali kwa wanafunzi na ushirikishwaji wa masuala ya Utalii.
Alisema Elimu hiyo imetolewa kwa lengo la kuwafanya wafahamu misingi na kanuni za uendeshaji bodaboda pamoja sheria za usalama barabarani. Pia katika kuwajengea uwezo Wanafunzi kulikuwa na kongamano kwa wanafunzi ambapo baada ya kongamano hilo wamepatikana washindi ambao wamepewa zawadi mbalimbali ikiwemo shajala, pamoja na kuwafungulia akaunti na kuwawekea akiba kwa kila mshindi.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa