• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIGODI iweke mitambo ya kuchenjulia madini

Tarehe ya kuwekwa: August 6th, 2018

NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewataka wamiliki wa migodi nchini kuhakikisha wanaweka mitambo ya kuchenjulia madini ili kuyaongezea thamani kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.Naibu Waziri Biteko ametoa wito huo kwenye mkutano wake na wachimbaji wadogo alioufanya katika kijiji cha Mbesa kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma mara baada ya kutembelea Mgodi wa Shaba wa Mbesa kama moja ya ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za madini katika mikoa ya Kusini ili kubaini changamoto pamoja na kuzitatua.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera, Mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya ya Tunduru.

Alisema kuwa, wamiliki wa migodi wanatakiwa kuhakikisha wanaweka mitambo ya kuchenjulia madini ili mbali na kuongeza mapato nchini watoe ajira kwa wananchi wanaozunguka migodi.Katika hatua nyingine, Biteko aliwataka wamiliki wa migodi kununua bidhaa za ndani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi pamoja na kutoa ajira kwa wazawa ili wananchi wanufaike na rasilimali za madini hayo.Pia aliwataka wamiliki wa migodi kuhakikisha wanasajili mikataba yao kwenye Ofisi za Wizara ya Madini kama Sheria ya Madini inavyotaka.

Awali wakiwasilisha changamoto mbalimbali kwa Naibu Waziri Biteko, wachimbaji hao walitaja kuwa ni pamoja na mitaji midogo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa madini, vifaa duni vya uchimbaji pamoja na leseni za madini kulipiwa kwa fedha za kigeni.Walitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa maabara za kupima madini migodini na baadhi ya wachimbaji kufutiwa leseni zao.

Wakati huo huo akielezea shughuli za uchimbaji madini ya shaba katika eneo la Mbesa lililopo Tunduru mkoani Ruvuma, Afisa Madini wa Tunduru Mjiolojia Abraham Nkya  alisema Serikali ilitenga eneo la Mbesa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 156.053 ambalo liko umbali wa takribani kilometa 66 kutoka Tunduru Mjini.

Alisema leseni nyingi zimekuwa hazifanyiwi kazi hali iliyopelekea leseni zaidi ya 1000 kufutwa.Aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa Mbesa ina jumla ya leseni 441 za wachimbaji madini wadogo ambazo kati ya hizo 158 ni hai na 283 zina makosa mbalimbali ikiwemo kutokulipa ada ya pango, kutowasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa kila robo mwaka n.k.

Akielezea faida za uchimbaji madini ya shaba katika kijiji cha Mbesa Mjiolojia Nkya alieleza kuwa ni pamoja na ulipaji wa kodi mbalimbali ikiwemo mrabaha, ajira kwa vijana wa kijiji cha Mbesa pamoja na vijiji vya jirani.Aliendelea kutaja faida nyingine kuwa ni pamoja na uchangiaji wa shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko, uchimbaji wa kisima katika shule ya sekondari ya Mbesa, hospitali na ajira kwa wakinamama wanaohudumia eneo la uchimbaji.

Imeandaliwa na:

Greyson Mwase, Tunduru

Afisa Habari,Wizara ya Madini

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa