Na;
Amina Pilly
25 Agost 2022.
Utekelezaji wa Mkopo umegawika katika sehemu kuu tatu ambazo ni mkopo wenyewe, urejeshaji na uzalishaji wake endapo utafanya marejesho ya mkopo wako ni sehemu ya utekelezaji wa mpango husika.
Kauli hiyo imetolewa na Mheshimiwa Mbunge Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro wakati akisimamia zoezi la ugawaji wa mkopo wa shilingi milioni 236 kwa vikundi vya wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2% ikiwa ni sehemu ya 10% fedha ya zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa Wilaya ya Songea tarehe 22 Agosti 2022.
Dkt. Ndumbaro (MB) alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10% kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuinua kipato cha jamii.
Amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi ya maendeleo ambayo inasaidia kukuza uchumi wa Taifa letu ambapo asilimia ya fedha hizo hurudi katika Halmashauri zetu hivyo huwasaidia wananchi kukopeshwa Mikopo ya bila riba kwa kupitia vikundi mbalimbali vya wajasiliamali wadogo wadogo. DKT. Ndumbaro Alisisitiza.

Mheshimiwa Mbunge ameahidi kutembelea vikundi vyote vilivyopewa Mkopo ndani ya mwaka wa fedha 2021 hadi 2022 ifikapo mwezi oktoba 2022 kwa lengo la kufanya uhakiki wa vikundi hivyo na kujiridhisha maendeleo ya vikundi mbalimbali vilivyopewa mikopo na Halmashauri.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema kuwa “ Lengo la Serikali katika ugawaji mikopo ya 10% ni pamoja na kuwaongezea kipato wananchi na kupunguza umaskini katika jamii. “
Amewarai wanavikundi wote kusimamia vizuri miradi yao ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na Halmashauri iweze kukopesha wanavikundi wengine.
Afisa Maendeleo ya jamii Martini Mtani amesema kuwa Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2021 hadi 2022 kiasi cha shilingi 356,700,000/= kutoka mapato ya ndani ambapo fedha hizo zimechangiwa katika mfuko wa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu
Mtani aliongeaza kuwa katika robo ya nne ya mwaka 2021 hadi 2022 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekopesha kiasi cha shilingi milioni 236,000,000/= kwa vikundi 15 vya wajasiliamali vyenye jumla ya wananchama 118 ikiwa vikundi vya wanawake wamepata milioni 100,000,000 kwa vikundi 6 vyenye wananchama 77, vikundi vya vijana kiasi cha shilingi milioni 113,000,000/= kwa vikundi 6 vyene wanachama 34, pamoja na vikundi vya watu wenye ulemavu kiasi cha shilingi milioni 23,000,000/= kwa vikundi vyenye wanachama 7.
Miongoni mwa vikundi hivyo vimetoka katika kata ya Mjimwema, Lilambo, Misufini, Matarawe, na Kata ya
Bombambili.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa