• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIL. 236 ZATOLEWA MKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU.

Tarehe ya kuwekwa: August 25th, 2022

Na;

Amina Pilly

25 Agost 2022.

Utekelezaji na uendeshaji wa Mkopo umegawika katika  sehemu kuu tatu ambazo ni mkopo wenyewe, urejeshaji na uzalishaji wake endapo  utafanya marejesho ya  mkopo wako   ni sehemu ya utekelezaji wa mpango husika.

 Kauli hiyo  imetolewa na Mheshimiwa Mbunge Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro wakati akisimamia zoezi la ugawaji wa mkopo wa shilingi milioni 236 kwa vikundi vya wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2% ikiwa ni sehemu ya 10%  fedha ya  zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa Wilaya ya Songea tarehe 22 Agosti 2022.


Dkt. Ndumbaro (MB) alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais  Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10% kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuinua kipato cha jamii.

Amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi ya maendeleo ambayo inasaidia kukuza uchumi wa Taifa letu ambapo asilimia ya  fedha hizo hurudi katika Halmashauri zetu hivyo  huwasaidia wananchi kukopeshwa Mikopo ya bila riba kwa  kupitia vikundi mbalimbali vya wajasiliamali wadogo wadogo. DKT. Ndumbaro  Alisisitiza.

Dkt. Ndumbaro (MB) alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais  Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10% kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuinua kipato cha jamii.

Amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi ya maendeleo ambayo inasaidia kukuza uchumi wa Taifa letu ambapo asilimia ya  fedha hizo hurudi katika Halmashauri zetu hivyo  huwasaidia wananchi kukopeshwa Mikopo ya bila riba kwa  kupitia vikundi mbalimbali vya wajasiliamali wadogo wadogo. DKT. Ndumbaro  Alisisitiza.



Mheshimiwa Mbunge ameahidi kutembelea vikundi vyote vilivyopewa Mkopo ndani ya mwaka wa fedha 2021 hadi 2022 ifikapo mwezi oktoba 2022 kwa lengo la kufanya uhakiki wa vikundi  hivyo na  kujiridhisha maendeleo ya vikundi mbalimbali vilivyopewa mikopo na Halmashauri.

Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema kuwa “ Lengo la Serikali katika ugawaji mikopo ya 10% ni pamoja na kuwaongezea  kipato wananchi  na kuondoa umaskini katika jamii. “

Amewarai wanavikundi wote kusimamia vizuri miradi yao ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na Halmashauri iweze kukopesha wanavikundi wengine.


Afisa Maendeleo ya jamii Martini Mtani  amesema kuwa Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha  2021 hadi 2022   kiasi cha shilingi 356,700,000/=  kutoka mapato ya ndani ambapo fedha hizo zimechangiwa katika mfuko wa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu

Mtani aliongeaza kuwa katika robo ya nne ya mwaka 2021 hadi 2022 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekopesha kiasi cha shilingi milioni 236,000,000/=  kwa vikundi 15 vya wajasiliamali vyenye jumla ya wananchama 118 ikiwa vikundi vya wanawake wamepata milioni 100,000,000 kwa vikundi 6 vyenye wananchama 77, vikundi vya vijana kiasi cha shilingi milioni 113,000,000/= kwa vikundi 6 vyene wanachama 34, pamoja na vikundi vya watu wenye ulemavu kiasi cha shilingi milioni 23,000,000/= kwa vikundi vyenye wanachama 7.

Miongoni mwa vikundi vilivyopata  mkopo awamu ya nne ni kutoka  kata  ya Mjimwema, Lilambo, Misufini, Matarawe, na Kata ya

 Bombambili.

Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa