Mwenyekiti wa CCM mkoa Oddo Mwisho ameongoza ziara ya kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma na kufanikiwa kutembelea Miradi Mbalimbali Manispaa ya Songea ikiwa ni utekelezaji wa ILANI ya chama cha Mapinduzi “CCM” iliyofanyika 08/07/2020.
Oddo akiwakilishwa na mjumbe wa Kamati kuu CCM Taifa Mussa Homera ambaye alianza kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo kwa usimamamizi mzuri wa Mradi wa Barabara ambayo imetekelezwa kwa kiwango kizuri na kwa wakati.
Alisema Pamoja na usimamizi mzuri wa Miradi Manispaa ya Songea, alimsisitiza Mkurugenzi huyo kuendelea kutengeneza barabara chakavu na zenye vumbi zilizopo katikati ya Mji ili kutekeleza mkakati wa “Ondoa Vumbi mjini“.
Alibainisha kuwa Miongoni mwa barabara muhimu iliyokuwa inahitaji matengenezo ya haraka kati ya Barabara zilizopo Manispaa ya Songea ni pamoja na barabara ya Tunduru JCT-SEEDFARM ambayo mara nyingi hutumika kupita wananchi na Wageni mbalimbali wakielekea kwenye nyumba za kulala Wageni/Hotel.”
Naye Maneja Tarura Manispaa ya Songea Eng Boniface Makiya alisema ujenzi wa Barabara ya Tunduru JCT-Seedfarm km. 0.75 ulianza rasmi 28/01/2020 na umekamilika 27/05/2020 ambao umegharimu jumla ya Tsh 334,038,500/= fedha kutoka Serikalini.
Eng. Makiya alifafanua kuwa mradi huo umejengwa na Mkandarasi Eima General Supplies LTD wa Songea ambapo ulihusisha kuchonga barabara na kushindilia, kuweka tabaka za changarawe, kuweka tabaka za Lami, pamoja na ujenzi wa mitaro ya zege ya maji ya mvua, Drift na karavati. Aliongeza kuwa Serikali imeleta fedha nyingine kwa ajili ya kuongeza Mita 500 za barabara ambazo zitatangazwa mwezi july 2020.
IMENDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI-MANISPAA YA SONGEA.
09/07/2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa