Mikopo hiyo imetolewa jana 09/07/2020 kwa wajasiliamali wadogo wadogo, iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ambaye aliwakilishwa na Afisa Tarafa Madaba Showin Mapunda.
Mapunda alisema “Manispaa ya Songea imetoa Mikopo kwa vikundi 28 vya wajasiliamali Wanawake, Vijana, na Wenye ulemavu jumla ya Tsh 51,020,000/= ikiwa ni sehemu ya makusanyo ya Mapato ya ndani ya Manispaa ya Songea kwa mgawanyo wa wanawake 4%, Vijana 4%, na Walemavu 2% sawa na 10%.
Alianza kwa kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa jitihada nzuri za utoaji wa Mikopo kwa makundi Maalmu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya awamu ya tano.
Alisema madhumuni na Shabaha kuu ya kuundwa kwa Vikundi hivi ni kujenga umoja katika utendaji wa Kazi na kudhaminiana ili kuwa na mafanikio ya haraka katika jamii.Hata hivyo aliwaasa wajasiliamali hao kutumia vizuri Mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia kukuza mitaji yao pamoja na Kipato cha Familia.
Alisema, sifa nzuri ya mkopaji ni kufanya marejesho kwa wakati ili waweze kukopesheka mara wanapohitaji mikopo. Aliongeza kuwa kutorejesha fedha kwa wakati ni kudidimiza uchumi wa Taifa kwa ujumla. Mikopo hiyo itaendelea kutolewa kila mwezi na bila riba yoyote.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KAIMU AFISA HABARI- MANISPAA YA SONGEA.
10.07.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa