MKUU wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba anasema milango ya utalii Mwambao mwa ziwa Nyasa tayari imeanza kufunguka ambapo hivi sasa watalii kutoka nchi mbalimbali ikiwemo barani Ulaya wanafika kutembelea wilaya hiyo yenye vivutio adimu vya utalii.
Anatoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwenda kuwekeza katika Wilaya ya Nyasa ambayo ina aina mbalimbali za maeneo ya uwekezaji na utalii.
Wawekezaji wa Kanisa katoliki ambao ni watawa wa Mtakatifu Vincent Jimbo la Mbinga tayari wamejenga hoteli ya kitalii yenye vyumba 35 ambayo imeanza kutumika na wageni wa ndani na nje ya nchi katika eneo la Kilosa nje kidogo toka Mbambabay makao makuu ya Wilaya ya Nyasa.
Akizungumza katika hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa ziwa Nyasa Mshauri na Mwakilishi wa Balozi wa Finland nchini Tanzania,Kari Leppanen anasema ameshangazwa na vivutio vya kipekee na adimu ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote Duniani vilivyopo katika ziwa hilo.
Anasisitiza kuwa iwapo vivutio hivyo vitaendelezwa vitafungua fursa za uwekezaji na utalii kwa wananchi wa eneo hilo na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla wake hali ambayo inaweza kutoa ajira kwa vijana na kupunguza umasikini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa