OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya ukarabati wa madarasa manne ya shule ya msingi Chandamali.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Keziah Katawa amesema shule hiyo,Desemba 2017 ilipata maafa ya kuezuliwa kwa paa la madarasa manne na ofisi mbili.
“Kuezuliwa kwa majengo hayo kunatokana uchakavu wa majengo ya shule yakiwemo madarasa,ofisi na vyoo’’,alisema Katawa.
Kulingana na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,kati ya fedha hizo,shilingi milioni nne zilitumika kupaua madarasa manne na ofisi mbili na shilingi 530,000 zilitumika kujenga kuta na ofisi zilizobomoka.
Katawa amebainisha Zaidi kuwa Zaidi ya shilingi milioni moja zilitumika kupaka rangi ndani ya madarasa na shilingi 200,000 zilitumika kutengeneza mlango wa ofisi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 3,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa